Watu wasiopungua 8 wamekufa baada ya kimbunga kilichopewa jina ´Grace´ kulipiga eneo la mashariki mwa Mexico na kusababisha mafuriko, maporomoko ya udongo na uharibifu mkubwa wa nyumba na biashara.
Kimbunga hicho kiliwasili Mexico kwa mara ya pili katika jimbo la Veracruz kikiambatana na upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita 200 kwa saa.
Katika jimbo hilo la Veracruz ambako kimbunga Grace kimefanya uharibifu mkubwa watu saba wamekufa na mwengine mmoja amepoteza maisha kwenye mji wa Poza Rica.
Mamlaka za jimbo la Veracruz zimesema zimeandaa maeneo 200 kwa ajili ya maakazi ya muda na kuwarai watu kwenda kwenye maeneo salama.
Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha huku akiarifu kikosi cha watu 8,000 kiko tayari kusaidia juhudi za uokoaji.

No comments:
Post a Comment