Search This Blog

Sunday, August 29, 2021

Uongozi wa Taliban wajiandaa kuunda baraza la mawaziri

 


Kundi la Taliban limesema linaunda baraza jipya la mawaziri wakati Marekani ikikaribia kukamilisha shughuli ya kuwaondoa watu na kwamba linatarajia kushuka kwa thamani ya fedha na kutokea mgogoro wa kiuchumi. 

Msemaji wa kundi hilo Zabihullah Mujahid ameliambia shirika la habari la Reuters, wakati shughuli hiyo ikitarajiwa kukamilika Agosti 31.

Mujahid amelaani mashambulio ya usiku kucha ya ndege za Marekani zisizoendeshwa na rubani dhidi ya wanamgambo wa kundi linalojiita dola la kiislamu IS kufuatia shambulio la Alhamisi la kujitoa mhanga karibu na uwanja wa ndege wa Kabul na kuita hatua hiyo kuwa mashambulio ya wazi katika ngome ya Afghanistan. 

Hata hivyo, ametoa wito kwa Marekani na mataifa mengine ya Magharibi kudumisha uhusiano wa kidiplomasia hata baada ya kuondoka kwao nchini humo, shughuli anayotarajia kukamilika karibuni.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...