Hatua ya kundi la Taliban kuchukuwa mamlaka nchini Afghanistan ilifunika mkutano ulioandaliwa jana mjini Baghdad uliowaleta pamoja viongozi wakuu wa kikanda pamoja na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliyeahidi kwamba nchi yake itabaki kuwa imara nchini Iraq.
Wakati wa mkutano huo ulioandaliwa na Iraq inayotafuta kutekeleza jukumu la mpatanishi katika kanda hiyo, Macron alisema kutokana na matukio ya kijiografia na kisiasa, mkutano huo umechukuwa mweleko maalumu na kwamba taifa lake litaendelea kuwapeleka wanajeshi wake nchini Iraq kukabiliana na ugaidi hata kama Marekani itawaondoa wanajeshi wake.
Mkutano huo unafanyika huku Iraq ambayo imeathirika kwa muda mrembo na ugaidi wa itikali kali, ikijaribu kujiimarisha kama mpatanishi kati ya Saudi Arabia na Iran.
Baada ya mkutano wa awali na waziri mkuu wa Iraqi Mustafa al-Kadhemi, Macron alisema wote wanafahamu kuwa hawapaswi kulegeza tahadhari yao kwa sababu kundi la Daesh lenye mafungamano na kundi linalojiita dola la kiislamu IS bado lni kitishio na anafahamu kuwa makundi hayo ya kigaidi ni kipaombele cha serikali hiyo.

No comments:
Post a Comment