Ripoti kubwa zaidi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi inatarajiwa kuchapishwa baadae, ikielezea uhalisia wa dunia ilivyo.
Utafiti huo umefanywa na jopo la serikali kuhusu mabadiliko ya tabia nchi- Umoja wa Mataifa umeangalia zaidi ya tafiti 14,000 za kisayansi.
Huu utakuwa utafiti mpya zaidi kuhusu ongezeko la joto na jinsi utakavyoleta mabadiliko duniani katika miongo ijayo.
Wanasayansi wanasema inawezekana kuwa si habari njema - lakini ikiwa na matumaini. Na wataalamu wa mazingira wamesema hii itaweza kuibua ari kwa serikali kupunguza uzalishaji.
Awali ripoti hiyo iliangalia sayansi ya ongezeko la joto mnamo mwaka 2013 - na wanasayansi wanaamini kuwa wamejifunza mengi tangu wakati huo.
Katika miaka ya hivi karibuni , dunia imeshuhudia joto likiwa limezidi, moto ukiwa umezidi na mafuriko kuongezeka.
Baadhi ya tafiti, zimeonesha kuwa mabadiliko yanayotokana na binadamu yanaweza yasibadilishwe kwa mamia au hata maelfu ya miaka.
Matokeo ya utafiti huo utatangazwa katika mkutano na waandishi wa habari na kutumiwa katika mkutano wa Novemba utakaofanyika Uingereza.
Mkutano wa COP26, unaoendeshwa na Umoja wa Mataifa- UN, unaonekana kuwa katika wakati mgumu kama mabadiliko ya tabia nchi yataenda kuthibitiwa.
Viongozi wa mataifa 196 watakutana na kujaribu kufikia katika utekelezaji.
Alok Sharma, waziri wa Uingereza ataongoja mkutano huo , alisema mwishoni mwa wiki kuwa dunia ni karibu inamaliza muda katika kuzuia majanga na - athari za mabadiliko ya tabia nchi tayari yameanza kuonekana.

No comments:
Post a Comment