Raia 12 waliuawa kwenye shambulizi la bomu lililotekelezwa katika mkoa wa Paktiya nchini Afghanistan.
Katika taarifa iliyotolewa na Idara ya Polisi ya Paktiya, iliripotiwa kuwa bomu lililonaswa barabarani katika kijiji cha Chinu cha wilaya ya Seyid Kerem mkoa huo kililipuliwa wakati gari lililokuwa limebeba raia lilikuwa likipita katika eneo hilo.
Ilielezwa kuwa raia 12, wakiwemo watoto, walipoteza maisha na raia 2 walijeruhiwa katika shambulizi hilo.
Idara ya Polisi ililaumu Taliban kwa kuhusika na shambulizi hilo.
Mpaka sasa bado hakuna mtu yeyote aliyedai kuhusika na shambulizi hilo.

No comments:
Post a Comment