Baada ya Maafisa wa Usalama wa GSU (General Service Unit) kuondolewa katika Makazi ya Naibu Rais wa Kenya, William Ruto, Ofisi ya Kiongozi huyo imesema kitendo hicho ni kinyume cha utaratibu
Imedaiwa kuwa ni mwendelezo wa jitihada za kudhoofisha Usalama Binafsi wa Naibu Rais kwasababu za kisiasa. Pia, ni mkakati unaotajwa kumuweka hatarini
Hata hivyo Jeshi la Polisi limesema Maafisa hao wamebadilishiwa majukumu na wengine (Government Building Unit) watalinda makazi ya Naibu Rais, utaratibu ambao ni wa kawaida kuongeza ufanisi

No comments:
Post a Comment