Search This Blog

Monday, August 23, 2021

Rais wa zamani aliyetaka kujiua jela "anaendelea vizuri"

 


Rais wa zamani wa Bolivia aliyeko jela Jeanine Anez anaendelea vizuri baada ya jaribio lake la kujiua kukwama.

Anez rais wa pili mwanamke Bolivia alijaribu kujiua baada ya waendesha mashitaka kumpa mashitaka ya "mauaji ya halaiki" kufuatia vifo vilivyotokea kwenye maandamano ya mwaka 2019, kwa mujibu wa taarifa.

Anez, 54, alitaka kujiua kwa sababu ya msongo wa mawazo na kutokana na kukaa mahabusu muda mrefu, alisema binti yake Carolina Ribera."Tunaweza kusema bila shaka kabisa kwamba, afya yake imeimarika," mkurugenzi wa magereza Juan Carlos Limpias, aliiambia reporters.Anez rais wa 66 wa Bolivia aliyetawala kwa muda kati ya 2019 na 2020 alikamatwa tangu mwezi Machi mwaka huu.

Siku ya jumamosi maafisa wa Bolivia walitangaza kwamba Anez alijaribu kujiua huku waziri wa mambo ya ndani Eduardo del Castillo akisema hakufanikiwa zaidi ya kupata michubuko kwenye mkono wake na anaendelea vizuri.Anez anadaiwa kula njama ya kufanya mapinduzi yaliyomuondoa rais Evo Molares madarakani, kufuatia wiki mbili za vurugu na maandamano.

Rais wa sasa wa Bolivia ni "swahiba" mkubwa wa Molares na wengi wanaona kukamatwa kwa Anez kunahusishwa na kisasi.Upinzani nchini humo umesikitishwa na namna Serikali inavyomtendea Anez na kutoa wito wa kuachiliwa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...