
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya na Kiongozi Upinzani nchini humo Raila Odinga ameunga mkono wito wa Rais wa taifa hilo Uhuru Kenyatta kuwa naibu wake William Ruto kujiuzulu kutoka serikalini iwapo hajaridhika na jinsi serikali inavyoendeshwa.
Odinga amesema hatua ya kuondoka serikalini kwa Ruto na wabaunge wanaomuunga mkono pamoja na chama cha UDA ndio jambo la ‘heshima’ kufanya kwa sasa.
“Iwapo unaona mambo hayako sawa na wewe ni mtu mwenye msimamo wako basi sema mambo sio mazuri na ujiuzulu’ Raila amesema.
''Kuna wabunge wanaosema kuwa wapo UDA ilihali wangali wanapokea mashahar akupitia chama cha Jubilee,wanafaa kujiuzulu na kuvitetea viti vyao kupitia chama kipya'' Aliongeza.
Kwa mara ya kwanza siku ya Jumatatu Rais Uhuru Kenyatta kupitia mahojiano ya runinga alimtaka naibu wake kuondoka serikalini badala ya kuikosoa kila mara.
Rais alisema Ruto anafaa kuzingatia kuendeleza kampeni zake za uchaguzi mkuu wa mwaka ujao akiwa nje ya serikali iwapo hajapendezwa na utawala wake.
Ruto hata hivyo hajaonyesha nia ya kutaka kuondoka serikalini na siku ya Jumanne alisema hataondoka kwenye serikali ambayo alisaidia kuiunda.
Ruto na Rais Kenyatta walishirikiana katika chaguzi za 2013 na 2017
No comments:
Post a Comment