Search This Blog

Monday, August 30, 2021

Nyumba 19 zateketea kwa moto Rufiji


Nyumba 19 zimeteketea kwa moto jana Agosti 29 katika kitongoji cha Shaurimoyo kijiji cha Nyamwage Kata ya wilayani, Rufiji Mkoani Pwani huku chanzo kikiwa ni Mwananchi mmoja kuwasha moto kwa ajili ya kusafisha eneo lake na kisha moto huo kuzidi na kumshinda kuuzima.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge na Wajumbe wa kamati ya usalama ya Wilaya ya Rufiji wamefika kwenye eneo la tukio ili kujionea athari na jitihada ambazo Uongozi wa Wilaya wamezichukua ili kuhakikisha Wananchi wanakuwa salama ambapo hata hivyo mbali na Wananchi kukosa makazi yao hakuna aliyefariki wala kujeruhiwa kutokana na moto huo.

RC Kunenge ametoa pole kwa Serikali ya Wilaya na Wananchi waliopatwa na moto huo hayo na kuwapongeza Wakazi wa maeneo ya karibu kuweza kuwapatia hifadhi Wananchi wenzao. 

Katika hatua nyingine RC Kunenge ameuagiza Uongozi wa Wilaya hiyo kufanya haraka uchunguzi ili kujua tathmini ya athari iliyopatikana ili kuweza kuwasaidia waliopata ajali hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya wa ya Rufiji Meja Edward Goweke amesema wananchi wapo salama na wote wamepata hifadhi kwa ndugu zao huku pia akiwataka kuwa makini pindi wanaposafisha maeneo yao na kuchoma moto.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...