
Mji wa Marekani wa New Orleans umepoteza umeme, majenereta pekee yakifanya kazi baada ya kimbunga Ida kupiga mji wa Louisiana.
Kimbunga hicho kilisababisha upepo wenye kasi ya kilomita 240 kwa saa kilipowasili na wale ambao hawakutoroka wameshauriwa kusalia ndani ya makazi.
Mtu mmoja alipoteza maisha yake baada ya mti kuangukia nyumba yao katika eneo la Ascension Parish. Ida kitajaribu kupiga maeneo yaliotengezwa ili kuzuia mafuriko baada ya kimbunga Katrina kuwaua takriban watu 1800 mwaka 2005.
Rais Joe Biden amesema kwamba Ida kitakuwa kimbunga kinachotishia maisha huku uharibifu mbaya ukitarajiwa kufanyika maeneo ya nchi kavu.
Zaidi ya takriban nyumba milioni moja mjini Louisiana hazina umeme, na bwana Biden amesema huenda ikachukua wiki kadhaa ili kuendelea na usambazaji wa bidhaa katika eneo hilo.
Rais ametangaza janga kubwa katika jimbo hilo , na kutoa ufadhili wa ziada ili kusaidia katika juhudi za uokoaji. Kimbunga Ida kilipata nguvu katika maji ya Ghuba la Mexico wikendi iliopita.
Kiliwasili kusini mwa Jimbo la New Orleans siku ya Jumapili kikitarajiwa kusababisha uharibifu mkubwa kwa makazi, miti na nyaya za umeme.
Huku kikiendelea , kasi ya upepe wake imepungua na kufikia 153 kwa saa na hivyobasi kuorodheshwa kama dhoruba ya awamu ya kwanza.
Katika maeneo mengine dhoruba hiyo huenda ikawa zaidi ya futi 16 kwa urefu , hali inayoziba maeneo mengi yalio chini katika pwani.
No comments:
Post a Comment