Mwanachama wa pili wa shirika moja la kupambana na ufisadi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekamatwa baada ya kutoa shutuma dhidi ya mke wa rais.
Shirika hilo, "Lutte Pour Le Changement" (Lucha) lilidai kwamba wakfu unaosimamiwa na Denise Tshisekedi ulikuwa umetumia vibaya misaada kwa ajili ya wahanga wa mlipuko wa volkano. Akfu huo ulikanusha madai hayo.
Ghislain Muhiwa alikamatwa nyumbani kwake katika mji wa mashariki wa Goma.
Mwenzake Parfait Muhani alikamatwa mnamo Julai juu ya tukio hilo na anasubiri kesi yake mbele ya korti ya kijeshi

No comments:
Post a Comment