Kamanda mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya,William Mkonda aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 12 jioni kwenye barabara itokayo Tarime kuelekea Nyamwaga.
Ajali hiyo ilihusisha kugonga magari mbalimbali ikiwemo waendesha pikipiki ambapo pikipiki yenye namba za usajili MC 708 CPC SANLG na dereva wake Samansi Magoiga walipata ajali kwa kugongwa na gari hilo.
"Gari lenye namba za usajili T166DJWMithshubishi lililo kuwa likiendeshwa na dereva wake Dickison Joseph mali ya Juma rashidi Mohamed wa Kahama Shinyanga lilipata ajali na kuuwa watu wawili,Jenifa Mbogo 11 mwanafunzi wa shule ya msingi Ronsoti pamoja na mwalimu Hamisi Mohamed 31 wa shule ya msingi Mturu na kujeruhi wengine watano baada ya kuferi bureki"alisema Mkonda.
Mkonda aliongeza kuwa marehemu wametambuliwa na hatua za mazishi zinaendelea ambapo majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya inayomilikiwa na halmashauri ya mji wa Tarime na majeruhi hao wanaendelea vizuri.
Kamanda huyo amewataja majeruhi kuwa ni Samansi Magoiga 30 mkazi wa Romoli halmashauri ya mji wa Tarime,Ibrahimu Mohamed 35 mkazi wa Kahama Sinyanga Jesca Joel 25,Sungura Joseph 56 mkazi wa Msati halmashauri ya mji wa Tarime na Jorodan Mujumi 25.
Mkonda amesema Dereva baada ya kusababisha ajali hiyo alitoroka kusiko julikana na polisi wanafanya jitihada za kumtafuta ili kwenda kujibu ukiukwaji wa sheria.
Kamanda huyo aliwataka watembea kwa miguu na watumiaji wa barabara kuwa makini ili kuepuka ajali ambazo hazina ulazima.

No comments:
Post a Comment