Search This Blog

Saturday, August 28, 2021

Muswada bima ya afya kwa wote kutua bungeni

 


Serikali ya Tanzania kupeleka bungeni muswada wa sheria ya bima ya afya kwa wote Septemba, 2021.


Hayo yamesemwa leo Jumamosi Agosti 28,  2021 na msemaji mkuu wa Serikali,  Gerson Msigwa wakati akifungua mkutano wa wahariri wa habari ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).


Msigwa amesema Serikali itaanza kutekeleza mpango wa bima ya afya kwa wote kwa kutenga Sh149 bilioni katika mwaka wa fedha 2021/22.


“Itaanza kwa makundi maalum kwa wale ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu lakini dhamira ya Serikali ni  hatua kwa hatua hatimaye Watanzania wote waweze kufikiwa,” amesema.


Amesema licha ya kuwa muswada haujawasilishwa bungeni,  Serikali kwa kutambua umuhimu iliamua kuanza kutenga fedha kwanza lengo ni sheria inapoanza kutekelezwa fedha ziwepo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...