Search This Blog

Saturday, August 28, 2021

KMC yajichimbia Morogoro, yagusia usajili mkubwa

 


Uongozi wa klabu ya Kinondoni Municipal Council ‘KMC’ umesema, Klabu inaendelea kufanya usajili na wakati wowote kwa utaratibu wa klabu utakapokamilika itaanza kuwatambulisha wachezaji wote ambao wamesajiliwa katika dirisha kubwa lililofunguliwa mapema Agosti mwaka huu.


KMC FC inawajulisha mashabiki, wapenzi na Watanzania kwa ujumla kuwa usajili unaoendelea kufanyika umezingatia matakwa ya mwalimu na kwamba inasajili wachezaji wenye viwango vya hali ya juu na bora watakaoleta manufaa makubwa katika timu hiyo.


Ikumbukwe kuwa Klabu ya KMC FC imeanza rasmi kambi mkoani Morogoro kwa ajili ya kujiandaa vizuri na msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania Bara 2021/2022 tokea Agosti 26 mwaka huu baada ya kuwasili mkoani humo asubuhi ya Agosti 25, 2021.


KMC FC ikiwa mkoani humo  kwa maandalizi hayo ya msimu mpya itakuwa na programu mbalimbali za mazoezi pamoja na kucheza mechi za kirafiki kama program inavyoonyesha kwa lengo la kuwapima na kuwaweka vizuri wachezaji kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu itakayoanza Septemba 27 mwaka huu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...