Search This Blog

Saturday, August 7, 2021

Moto mkubwa waendelea kuteketeza misitu ya Ugiriki, maelfu wahamishwa


Moto wa msituni umeendelea leo kuyateketeza maeneo makubwa yaliyobaki katika misitu ya Ugiriki na kuyafikia maeneo ya makazi baada ya kuharibu nyumba, biashara na mashamba. 


Katika nchi jirani Uturuki, moto ulioelezwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miongo mingi umeyateketeza maeneo ya pwani ya kusini mwa nchi hiyo kwa siku kumi zilizopita, na kuwauwa watu wanane. 


Askari mmoja wa zima moto wa kujitolea amefariki leo, wakati wengine 20 wakijeruhiwa baada ya moto mkubwa kuiteketeza sehemu kubwa ya mbuga kuu ya kitaifa katika mji mkuu wa Ugiriki, Athens. Maelfu ya wakaazi na watalii wamekimbia kwa kutumia magari na boti. 


Vikosi vya zima moto na ndege vimewasili nchini humo kutoka Ufaransa, Ukraine, Cyprus, Croatia, Sweden na Isrel, huku vingine zaidi vikitarajiwa kuwasili leo kutoka Romania na Uswisi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...