Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi ameyatolea wito mataifa ya Ulaya kuwasaidia wakimbizi wa Afghanistan ili kuepuka mzozo mkubwa wa wahamiaji kwenye kanda hiyo.
Grandi ameliambia gazeti moja ya kila siku la nchini Italia kwamba siyo rahisi kwa Ulaya kushuhudia wimbi la wakimbizi wa Afghanistan lakini hilo linategemea aina ya msaada utakaotolewa na kanda hiyo kwa wale watakaoikimbia Afghanistan kwenda mataifa jirani.
Mkuu huyo wa UNHCR amesema mataifa yatakayoandamwa na idadi kubwa ya wakimbizi wa Afghanistan ni pamoja na Pakistan, Iran na Tajikistan na Ulaya itapaswa kuwasaidia huko waliko kabla hawajafanya safari kukimbia mazingira magumu.
Wito wa Grand unafanana na ule uliotolewa na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliyewahimiza viongozi wa Ulaya kubeba dhima ya kuwasaidia wakimbizi wa Afghanistan ili kuepuka mzozo wa wahamiaji kwenye mataifa ya bara hilo.
No comments:
Post a Comment