Search This Blog

Friday, August 27, 2021

Mbaroni kwa mauaji ya walinzi wawili


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia mtuhumiwa mmoja Mohamed Jumaa (37) mkazi wa Kariakoo kwa mauaji ya walinzi wawili wa Kampuni ya Ulinzi ya Lock Fort Security, Eliakim Morali (30) na Saunkoo (35) Bakari.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Muliro Jumnne mtuhumiwa huyo inadaiwa aliwaua walinzi hao jana Agosti 26 ,2021 katika eneo la Tungi, Kigamboni kwa kuwagonga na Lori kwa makusudi.

Kamanda Muliro amesema taarifa zinaonesha mtuhumiwa huyo alishindwa kesi ya madai mahakama Kuu iliyofunguliwa na Benki ya Access baada ya kushindwa kulipa mkopo aliochukua katika Benki hiyo kwa wakati na kutolewa amri ya kuuzwa kwa kituo chake cha mafuta cha JM Petrol Station kilichopo Kigamboni.
 

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...