Search This Blog

Tuesday, August 3, 2021

Mapigano yapamba moto, Taliban washambulia mji muhimu Afghanistan


Mapigano makali yanaendelea katika mji mkubwa wa Afghanistan, huku kukiwa na hofu kuwa huenda ukawa mji wa kwanza kuangukia mikononi mwa Taliban.

Lashkar Gah katika mji wa kusini mwa jimbo la Helmand liko mwenye mashambulizi makali kutoka kwa wanamgambo, licha ya mashambulio ya angani ya Marekani na Afghanistan.

Taliban wanasemekana kukidhibiti kituo cha runinga. Maelfu ya watu waliokimbia maeneo ya vijijini walikimbilia katika majengo.

"Kuna mapigano pande zote," daktari aliiambia BBC kutoka kwenye hospitali yake.

''Hivi si vita vya Afghanistan, hivi ni vita kati ya uhuru na udikteta,'' alisema Meja Jenerali Sadaat alipozungumza na BBC.

Jumatatu, wizara ya habari nchini Afghanistan ilitangaza kuwa redio 11 na televisheni nne katika jimbo la Helmand ziliacha kutangaza kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ''mashambulizi na vitisho'' vya Taliban.

Majaribio ya wanamgambo kudhibiri Kandahar, mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, yameendelea baada ya mashambulizi ya roketi kupiga uwanja wa ndege wa mji huo Jumapili.

Kuunyakua mji wa Kandahar itakuwa ishara kubwa ya ushindi wa Taliban, na kuwapa nguvu kusini mwa nchi hyo.

Katika mji wa tatu uliozingirwa wa Herat, upande wa magharibi, makomandoo wa serikali wanapambana na wanamgambo. Vikosi vya serikali vimechukua maeneo kadhaa kutoka mikononi mwa waasi baada eneo la majengo ya Umoja wa Mataifa kushambuliwa Ijumaa.

Video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimeonesha wakazi kwenye mitaa na waliokuwa juu ya paa wakitamka kwa ngungu ''Allahu akbar'' (Mungu ni mkubwa) wakiunga mkono mafanikio ya serikali.

Wakati vikosi vya serikali vikipambana kurejesha maeneo yanayodhibitiwa na Taliban, Rais Ashraf Ghani amelaumu kuondoka kwa vikosi vya Marekani ambako kumezidisha mapigano nchini humo.

''Sababu ya hali tulionayo sasa ni kuwa uamuzi ulichukuliwa ghafla, '' aliliambia bunge.

Bw. Ghani amesema aliipa angalizo Washington kuwa kuondoka kutasababisha ''madhara''.

Ingawa karibu vikosi vyote vya kijeshi vimeondoka, Marekani imeendelea na mashambulizi ya anga kuyasaidia majeshi ya serikali. Mashambulizi yanayolenga mji wa Lashkar Gah yaliendelea mpaka usiku wa Jumatatu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...