Search This Blog

Wednesday, August 18, 2021

Maombolezo ya siku mbili yatangazwa Niger


S
iku mbili za maombolezo ya kitaifa zilitangazwa kote nchini Niger baada ya shambulizi la kigaidi kutokea katika mpaka wa Mali na Niger, ambapo watu 37 walipoteza maisha.

Katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na Msemaji wa Serikali Abdoulkadri Tidjani, ilielezwa kuwa masaa 48 ya maombolezo ya kitaifa yalitangazwa kuanzia jana usiku.

Katika shambulizi la kigaidi lililotekelezwa mnamo Agosti 16 na watu wasiojulikana katika kijiji cha Darey Dey kilichoko mkoa wa Tillaberi, watu 37, wakiwemo watoto 14, wanawake 4, walipoteza maisha.

Kijiji cha Darey Dey pia kilikumbwa na mashambulizi mnamo Julai 26, na raia 16 waliuawa.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...