Na Timothy Itembe Mara.
JAMII imetakiwa kujiinua kupitia fedha zainazotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF.
Akiongea Afisa Tarafa Inchage,Jonadhani Machango kwenye ufunguzi wa kikao kazi cha kujenga uwelewa kuhusu sehemu ya pili ya awamu ya tatu ya TASAF.
Kikao hicho kiliwashirikisha Viongozi watendaji na wawezeshaji kilichokalia ukumbi wa shule ye sekondari Tarime chenye lengo la kuwajengea uwelewa kuhusu kipindi cha pili awamu ya Tatu ya TASAF.
Machango alisema kuwa mfuko huu unalengo la kupambana na umasikini ambayo yalianzatu baada ya kujipatia Uhuru mpango wa TASAF ni moja ya jitihada za kupambana na umasikini.
"Tunapoongea na walengwa kunahitajika kutenga mda wa kuwashawishi wanapopokea fedha hizi za Ruzuku kuanzisha miradi badala ya kuzitumia kwa matumizi ya kibinafsi ambayo hayaleti tija kwenye familia na serikali kwaujumla"alisema Machango.
Afisa huyo aliomba uzalendo utumike katika upatikanaji wa walengwa kuwa ni wale ambao wanakidhi vigezo.
Mfuko huo unalengo la kunusuru kaya masikini ambapo jamii pia imetakiwa kubuni miradi ya kijamii na kuwa wakipewa na kuchukua fedha hizo wajikite katika matumizi bora kama vile elimu na Afya kwenye falima zenu aliongeza kusema Machango.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Tarime,Daniel Komote aliomba madiwani kushirikishwa katika mpango huo tangu hatua za awali ili kufanikisha mpango.
Naye Changa Wamba Makoba ambaye ni msimamizi wa zoezi la utambuzi ya uwandikishaji wa kaya za walengwa kupitia TASAF 111(awamu ya 11) alisema kuwa madhumuni ya kipindi hiki kuwezesha kaya za walengwa kutumia frusa za kuongeza kipato,huduma za kijamii na kuwekeza katika kuendeleza watoto wao.
Kiongozi huyo aliongeza kusema kuwa kuwekeza katika watoto ili kuleta matokeo chanya yatakayo dumu kwa mda mrefu kielimu na kiafya.
Patrice Bonfhace mratibu wa TASAF halmashauri ya Mji wa Tarime alisema kuwa walengwa watakao tambuliwa na kuandikishwa katika kipindi cha pilli ni kaya zinazoishi katika hali duni kwenye vijiji mitaa na sheria zetu.
Afisa huyo aliongeza kusema wanufaika ndani ya kaya ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 wanaohudhuria kiliniki wanafunzi wa shule za awali shule za msingi na shule za sekondari mama mjamzito namwanakaya mwenye ulemavu na kuwa mpango unatoa ruzuku za aina mbili ruzuku ya msingi na ruzuku ya masharti kwa wale ambao wanatakiwa kwenda shuleni na watoto wanaohudhuria kliniki.
Pia Afisa huyo alisema kuna ajira za mda zitolewazo kwa mwanakaya mmoja ambaye anauwezo wa kufanya kazi ambapo aliomba ushirikiano katika utekelezaji wa zoezi..

No comments:
Post a Comment