Search This Blog

Saturday, August 28, 2021

Iran yalaani mashambulizi ya kigaidi Afghanistan


Iran imelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyoua makumi ya watu huko Kabul, mji mkuu wa Afghanistan.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Said Hatibzade, alielezea masikitiko yao makubwa kwa mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea Afghanistan.

Akisisitiza kwamba wanalaani kila aina ya vitendo vya kigaidi dhidi ya watu wa Afghanistan, Hatibzade alisema kuwa serikali inayojumuisha inapaswa kuanzishwa haraka iwezekanavyo na taasisi zinazohusika na usalama zinapaswa kulinda maisha na mali ya watu.

Milipuko miwili tofauti ilitokea jana katika eneo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai huko Kabul, ambapo shughuli za uhamishaji zinaendelea. Kundi la Khorasan linalofungamana na shirika la kigaidi la DAESH lilidai kuhusika na mashambulizi hayo.

Kulingana na habari za Al-Jazeera, watu wasiopungua 110, 13 kati yao wakiwa ni wanajeshi wa Marekani walipoteza maisha kwenye mashambulizi ya kigaidi hadi kufikia sasa.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...