Search This Blog

Friday, August 20, 2021

Halmashauri kuu CCM Masasi yaridhishwa na utekelezaji ilani ya CCM


Na Hamisi Nasri, Masasi

HALMASHAURI kuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Masasi mkoani Mtwara imesema kuwa imeridhishwa na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho kutokana na serikali kutekeleza miradi mingi ya maendeleo wilayani Masasi kwa ufanisi.

Hayo yalielezwa jana mjini Masasi na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Masasi,Edward Mmavele alipokuwa akizungumza na wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya hiyo, ambapo halmashauri kuu hiyo imepokea rasmi taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha Januari hadi Juni kwa mwaka 2021

Mmavele alisema halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Masasi imeridhia kwa dhati kuipokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi inayotekelezwa na serikali wilayani Masasi kwa sababu kufuatia kamati ya siasa ya wilaya kufanya ukaguzi katika baadhi ya miradi ya maendeleo na kukuta miradi hiyo imetekelezwa kwa ufanisi.

Alisema kuwa licha ya kupokea taarifa hiyo na kuridhishwa utekelezaji wake ila ipo baadhi ya miradi ya maendeleo ambayo imekutwa ikiwa imetekelezwa chini ya kiwango na hata matumiz ya fedha zilizotumika haziendani na ubora wa miradi iliyotekelezwa ambapo baadhi ya watendaji wa serikali pamoja na taasisi wamekuwa chanzo cha miradi hiyo kutekelezwa chini ya kiwango.

 Mmavele alisema aidha halmashauri kuu ya CCM inaiushauri serikali kuendelea kuitekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa umakini katika kuwahudumia wananchi kwa kutekeleza miradi ya maendeleo kuendana na thamani halisi ya fedha za serikali ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo kwenye maeneo yao.

 Alisema kabla ya kuelekea katika mkutano wa halmashauri kuu ya CCM wilaya kamati ya siasa wilaya ilifanya ukaguzi maalumu wa miradi ya maendeleo ili kujionea hali ya utekelezaji wa miradi hiyo na katika ukaguzi huo miradi mbalimbali ilipitiwa na kufanyiwa ukaguzi ikiwemo mradi wa ujenzi wa hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Masasi, kituo cha afya Mbondo ambacho ktuo hicho kilifunguliwa na hayati, rais Dk. John Magufuli.

 Mmavele alisema katika ukaguzi huo changamoto kubwa iliyobainika ilikuwa katika kituo cha afya mbonde ambapo walikuta kituo hicho kinakabiliwa na ukosefu mkubwa wa vifaa tiba ikiwemo Xray hali inayochangia utoaji wa huduma za afya kuzorota kwa wananchi.

Alisema katika ukaguzi huo kamati ya siasa ilipitia katika miradi ya sekta ya zote elimu, afya,maji na miundombinu ya barabara na kujiridhisha na hali ya utekelezaji wake ambapo watendaji ni wazi kabisa wamefanya kazi kubwa kwa niaba ya serikali hivyo wananchi kwa sehemu wamenufaika na miradi hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Masasi,Claudia Kitta ambaye pia ni mjumbe wa mkutano huo alisema kazi kubwa ya ushirikiano katika kusimamia imara ilani ya uchaguzi ya CCM inapaswa kuwa na ushirikiano wa bega kwa bega baina ya watendaji, wananchi na viongozi wa vyama vya siasa ikiwemo chama cha mapinduzi kinachosimamia ilani hiyo wilayani humo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...