Search This Blog

Tuesday, August 24, 2021

DC apiga marufuku vimini wilayani kwake


Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, amepiga marufuku mavazi yasiyo na staha ikiwemo vimini na suruali za milegezo wilayani kwake na amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Nyasa, kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote watakao vaa mavazi ya namna hiyo.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na kujibu kero za wananchi wa Kijiji cha Lulimbo wilayani humo, ambapo pia akakemea tabia ya wanaume wanaopiga wake zao na kuwataka wabadilike la sivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

"Wanyasa ni wastaarabu bwana, hata wakiwa wanacheza Mganda wanavaa nguo nyeupe na hazichafuki hata wakicheza masaa na masaa, nguo fupi na Milege Hazitakiwi wilayani Nyasa," amesema Mkuu wa Wilaya.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...