Marekani na baadhi ya washirika wake wameshindwa kuafikiana juu ya msimamo wa Rais Joe Biden wa kusisitiza Agosti 31 kama muda wa mwisho wa kuondoa vikosi vyake vya usalama nchini Afghanistan, hatua ambayo itafunga kabisa zoezi la kuwahamisha watu kutoka Kabul.
Biden ameshikilia msimamo wake baada ya mazungumzo na viongozi wa mataifa yaliyoendelea kiuchumi duniani G7, kuwa Marekani na washirika wake wa karibu watasimama bega kwa bega siku za usoni juu ya kadhia ya Afghanistan.
Uingereza na washirika wengine wa G7 wamemtolea mwito Rais Biden kuwabakisha wanajeshi wa Marekani katika uwanja wa ndege wa Kabul kwa muda mrefu zaidi.
Maafisa wamesema hakuna nchi yoyote ambayo itaweza kuwahamisha raia wake wote kufikia muda wa mwisho wa Agosti 31.
Biden hata hivyo amesisitiza juu ya kitisho cha kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi iwapo Marekani itaridhia ombi la viongozi wa G7 la kutaka wanajeshi 5,800 wa Marekani waendelee kubakia Afghanistan baada ya muda wa mwisho wa Agosti 31.

No comments:
Post a Comment