Search This Blog

Wednesday, August 25, 2021

Afghanistan: Taliban yawaagiza wanawake wanaofanya kazi kusalia nyumbani


Wanawake wanaofanya kazi nchini Afghanistan lazima wabaki nyumbani hadi mifumo sahihi itakapowekwa kuhakikisha usalama wao, msemaji wa Taliban amewaambia waandishi wa habari.

"Ni utaratibu wa muda mfupi," msemaji Zabihullah Mujahid alisema. Taliban, ambao walitekelewza sharia kali za kiislamu wakati walipokuwa wakiongoza Afghanistan kabla ya 2001, walichukua udhibiti kamili wa nchi hiyo siku tisa zilizopita.

UN imeangazia ripoti "za kuaminika" za dhuluma za Taliban, haswa vikwazo dhidi ya wanawake.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet alisema Jumanne kwamba haki za wanawake ni "Mstari mwekundu’ ambao Taliban hawafai kuvuka.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari huko Kabul Jumanne, msemaji wa Taliban pia alizungumzia uokoaji unaoongozwa na Marekani kutoka mji mkuu, Kabul.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...