Search This Blog

Tuesday, August 24, 2021

Afghanistan: Marekani yashinikizwa kuongeza muda wa kuwaokoa watu


Marekani inashinikizwa kuruhusu muda zaidi wa uokoaji kutoka Afghanistan katika maeneo yanayodhibitiwa na Taliban wakati tarehe ya mwisho ya kujiondoa ikikaribia.

Chini ya makubaliano na Taliban, Marekani lazima iondoke ifikapo tarehe 31 Agosti. Lakini Ufaransa, Uingereza na Ujerumani zote zilielezea uwezekano wa kuruhusu muda zaidi kabla ya mkutano huo Jumanne.

Rais wa Marekani Joe Biden yuko tayari kuamua ndani ya saa 24 ijayo ikiwa ataongeza muda wa kujiondoa, afisa mmoja aliliambia shirika la habari la Reuters.

Walakini Taliban wameiambia BBC kwamba nyongeza yoyote ya muda itakiuka makubaliano yaliyokubaliwa na kuonya juu ya athari ikiwa vikosi hivyo vitabaki.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...