Search This Blog

Saturday, July 17, 2021

Yanga yatuma salamu Dodoma Jiji "Hatujamaliza ligi bado"


 RAZACK Siwa, Kocha wa Makipa wa Yanga ameweka wazi kuwa timu hiyo bado haijamaliza ligi hivyo katika mechi zao watakazocheza watapambana kupata pointi tatu. 

Kesho, Julai 18 Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassreddine Nabi itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Jamhuri,  Dodoma.

Mchezo wake uliopita kilishinda mabao 2-0 mbele ya Ihefu ambapo mabao yote yalifungwa na Feisal Salum

Tayari kikosi hicho kimeshatia timu Dodoma ilikuwa ni jana Julai 16 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa kwanza Yanga ilishinda mabao 3-1 na kusepa na pointi tatu muhimu. 

Siwa amesema:"Bado tunaendelea kupambana na ligi kwetu haijaisha hivyo mechi zetu tutacheza kwa nidhamu tukihitaji ushindi,".

Ikiwa nafasi ya pili na pointi 73 inakutana na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 7 na pointi 43.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...