Na Ahmad Mmow, Nachingwea.
Katika kudumisha amani, upendo na mshikamano katika jamii. Mkuu wa wilaya ya Nachingwea ametoa rai kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuzipatia ufumbuzi dosari zinazoweza kusababisha migogoro.
Komba alitoa wito huo jana katika mtaa wa Tunduru ya leo, mamlaka ya mji mdogo wa Nachingwea alipozungumza na wananchi baada ya kusikiliza malalamiko ya baadhi ya wananchi yanayohusu ardhi.
Komba ambaye alikwenda katika mtaa huo na wataalamu wa kitengo cha ardhi cha halmashauri ya wilaya ya Nachingwea alisema jamii inakila sababu ya kuzitafutiasuluhisho dosari ndogo ndogo zinazojitokeza kabla hazija geuka nakuwa migogoro.
Alisema nijambo jema jamii ikatambua kwamba migogoro siyo ufahari. Kwahiyo kila mmoja aipuke vitendo vinavyoweza kusababisha migogoro.
Kwani mahali palipo na migogoro hapawezi kuwa na upendo, mshikamano na utulivu.
'' Migogoro siyo fahari, huwezi kupata ufahari kwakupenda migogoro. Ishini kama ndugu, mpendane na msaidiane mkitambua kwamba duniani tunapita tu,'' alisisitiza Komba.
Alisema tofauti ndogo ndogo baina ya mtu na mtu zinatakiwa kusuluhushwa na wahusika kwa kutumia hekima na busara badala ya kukuza na kuisubiri serikali ikatue migogoro hiyo ambayo kimsingi jamii yenyewe inaweza kutatua.
Komba ambaye ametengeneza utaratibu wa kusikiliza malalamiko na kero mbalimbali kila siku ya Jumatano na kwenda maeneo mbali mbali kujiridhisha baada ya kupokea na kusikiliza malalamiko ya wananchi alisema wananchi wanaposhindwa kutatua migogoro yao watarajie serikali itashughulikia kwa mujibu wa sheria, taratibu na miongozo.
Komba aliwasisitiza wananchi hao waone fahari kushiriana na kupendana ili wajiletee maendeleo yanayotokana na umoja kuliko mifarakano itakayodumaza maendeleo.
Aliwataka watumishi wa umma kushughulikia changamoto kwa wakati na watimize wajibu wao kwa kutenda haki.

No comments:
Post a Comment