Waziri wa Ulinzi wa zamani wa Marekani, Donald Rumsfeld amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88. Rumsfeld alihudumu nafasi hiyo wakati wa uongozi wa Rais George W Bush na ndiye aliyepanga mipango ya Marekani kuingia kijeshi Afghanistan na Iraq.
Ramsfeld aluhudumu katika nafasi ya uwaziri wa ulinzi mara mbili. Mara ya kwanza ilianzia 1975 hadi 1977 chini ya Rais Gerald Ford na nyingine kuanzia 2001 hadi 2006, akichukua jukumu muhimu la ulinzi wa Marekani wakati wa mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11.
Kiongozi huyo alianza safari yake ya kisiasa 1963, pale alipochaguliwa kuingia katika Baraza la Wawakilishi la Marekani kupitia tiketi ya jimbo la Illinois.

No comments:
Post a Comment