Watu 2 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na ajali ya helikopta aina ya "MI-2" iliyotokea katika mkoa wa Nikolayevsk nchini Ukraine.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Huduma ya Dharura ya Ukraine, helikopta aina ya "MI-2" ilianguka karibu na kijiji cha Zayve katika mkoa wa Nikolayevsk.
Rubani pamoja na msaidizi wake walifariki baada ya helikopta hiyo iliyoanguka kuwaka moto.
Chanzo cha ajali ya helikopta bado kinachunguzwa.

No comments:
Post a Comment