Msemaji wa wizara ya kigeni wa Iran Saeed Khatib-zadeh, amesisitiza kuwa mpango wa ubadilishanaji wafungwa umefikiwa kati Jamhuri hiyo ya Kiislamu na Marekani, ikiwa ni siku moja baada ya Marekani kukanusha habari hiyo.
Khatib-zadeh amesema mpango huo ulikubaliwa na Marekani pamoja na Uingereza mjini Vienna, pembezoni mwa mkutano wa makubaliano ya pamoja ya utekelezaji wa mpango wa nyuklia unaofahamika kama JCPOA, kwamba wafungwa 10 wataachiliwa kutoka pande zote mbili na kwamba Iran iko tayari kutekeleza jukumu lake hii leo.
Iran na Marekani zimekuwa zikijadiliana kuhusu ubadilishanaji wa wafungwa, unaonuiwa kuachiwa huru kwa raia wa Iran wanaoshikiliwa Marekani na mataifa mengine kufuatia ukiukwaji wa vikwazo vya Marekani na pia kuachiwa huru kwa raia wa Marekani waliofungwa nchini Iran kwa makosa ya udukuzi.

No comments:
Post a Comment