Search This Blog

Wednesday, July 28, 2021

Wanasayansi wahimiza dharura ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi


Takribani miaka miwili baada ya zaidi ya wanasayansi 10,000 kutoka mataifa 150 kwa pamoja kutangaza dharura ya kushughulikia athari za mabadiliko ya tabia nchi, wameurejea tena wito wao na kutaka uharaka wa utatuzi wa kitisho hicho. 
 
Kwa mujibu wa jarida la kisayansi la BioScience, wanasayansi hao wanasema mabadiliko yanahitajika haraka sana kwa kuulinda uhai na dunia. Azimio lililosainiwa awali na wanasayansi 11,000 kwa sasa limengezewa nguvu na saini nyingine 2,800.
 
Tangu kusainiwa kwake kwa mara ya mwanzo azimio hilo la dharura la kimazingira 2019, kumetokea majanga kadhaa ya mafuriko, majanga ya moto ya misituni na ongezeko la joto, jambo ambalo linaonesha wazi ongezeko la athari za kimazingira duniani.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...