Search This Blog

Saturday, July 24, 2021

Wabunge Sierra Leone waunga mkono kufutwa adhabu ya kifo


Wabunge wa Sierra Leone jana walipiga kura kufuta adhabu ya kifo, na kuifanya kuwa nchi ya hivi karibuni barani Afrika kupiga hatua katika kuondokana na adhabu hiyo. 

Wabunge wengi walipiga kura ya kuunga mkono marekebisho ya kufuta adhabu ya kifo na badala yake itabadilishwa na kifungo cha maisha jela au miaka si chini ya 30 kwa mauaji. 

Sierra Leone haijawahi kutekeleza adhabu ya kifo tangu mwaka 1998, na na mara nyingi adhabu hiyo imekuwa ikipunguzwa. 

Nchi hiyo ambayo ndio kwanza inapona majeraha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, imekabiliwa na ukosoaji kutoka kwa makundi ya haki za binadamu kwa kuendelea kuwa na adhabu ya kifo. 

Mnamo mwezi Mei, naibu waziri wa sheria Umaru Napoleon Koroma alitangaza kuwa serikali inakusudia kuifuta adhabu ya kifo ili kuheshimu haki za binadamu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...