Search This Blog

Thursday, July 15, 2021

Viongozi kutuma video mkutano wa UN


Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekubaliana kuwaruhusu viongozi wa dunia kutuma tena taarifa zao kwa njia ya video badala ya kusafiri kwenda New York kuhudhuria mkutano wa mwaka utakaofanyika Septemba 21.

 Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Florencia Soto Nino amesema jana kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na janga la COVID-19. 

Mkutano wa mwaka huu wa viongozi wa dunia utatumia mfumo unaowaruhusu viongozi kuhudhuria ana kwa ana na kutoa hotuba zao na wengine wataziwasilisha kwa njia ya video. 

Nino amesema hilo linafanyika kwa sababu viwango vya chanjo ulimwenguni vinatofautiana na maambukizi ya aina mpya ya virusi vya corona yanasababisha wasiwasi. 

Nino amesema baraza hilo litafanya kazi kwa kufuata miongozo iliyotolewa na maafisa wa New York ya kupambana na virusi vya corona.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...