Search This Blog

Wednesday, July 14, 2021

UN: Idadi ya vifo vya wahamiaji yaongezeka mara 2


Shirika la Umoja wa Mataifa la Wahamiaji, IOM, limesema idadi ya wahamiaji na wakimbizi waliokufa wakati wakijaribu kuingia Ulaya kupitia baharini, imeongezeka mara mbili kwa mwaka huu ikilinganishwa na miezi sita ya kwanza ya mwaka 2020. 

Hayo yamebainishwa katika ripoti mpya ya IOM iliyotolewa jana. Shirika hilo limesema takribani watu 1,146 wamekufa kati ya mwezi Januari na Juni. IOM imesema idadi ya watu wanaosafiri kwenda Ulaya kupitia baharini pia imeongezeka kwa asilimia 56. 

Njia kuu ya Bahari ya Meditaranea kati ya Libya na Italia ndiyo iliyosababisha vifo zaidi, ambapo watu 741 walikufa. Watu 250 walikufa kupitia njia ya Bahari ya Atlantiki kati ya Afrika Magharibi na Visiwa vya Canary vilivyopo Uhispania.

Watu wapatao 149 walikufa kupitia njia ya eneo la Magharibi la Bahari ya Meditaranea kuingia Uhispania. Na wengine sita walikufa kupitia Mashariki mwa Bahari ya Meditaranea kuelekea Ugiriki.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...