Search This Blog

Wednesday, July 14, 2021

Mkuu wa UNICEF amejiuzulu wadhifa wake


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres, amekubali barua ya kujiuzulu kwa Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto, UNICEF Henrietta Fore. Kiongozi huyo anaondoka katika nafasi hiyo kutokana na sababu binafsi.

 Gutteres amesema ameipokea barua hiyo kwa masikitiko makubwa na amempongeza Fore kutokana na uongozi wake uliotukuka. Fore, mwenye umri wa miaka 72 amesema anaachana na majukumu hayo ili atumie muda wake zaidi kumuuguza mume wake ambaye anasumbuliwa na matatizo makubwa ya kiafya.

 Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq amesema Guterres anaelewa kabisa uamuzi wa Fore kujitoa kwa ajili ya familia yake. Katibu huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Fore atabakia madarakani hadi mrithi wake atakapopatikana.

 Fore, ambaye ameiongoza UNICEF tangu mwaka 2018 amesema kuwahudumia watoto wa ulimwengu ni jambo la kusisimua na kuvutia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...