Search This Blog

Saturday, July 3, 2021

Tetesi za soka kimataifa

 


Beki Sergio Ramos, 35, ambaye amemaliza mkataba wake na Real Madrid hivi karibuni amekataa ofa ya pauni milioni 10 ili kujiunga na klabu ya Manchester United. Ramos sasa anatarajiwa kujiunga na PSG kwa mkataba wa miaka miwili. (Mirror)

Arsenal pia wanafuatilia mwenendo wa mazungumzo baina Ramos na PSG wakiwa na nia ya kutangaza dau lao endapo mazungumzo hayo yatakwama. (Goal)

Mlinda mlango nambari moja wa Manchester United, David de Gea, 30, anapanga kusalia Old Trafford licha ya kuendelea kupata upinzani kutoka kwa makipa wengine. Upinzani unatarajiwa kuongezeka baada ya kipa Tom Heaton, 35, kurejea kutoka Aston Villa alipokuwa kwa mkopo. (Times - subscription required)

Klabu za Tottenham na Arsenal sasa zina nafasi nzuri ya kumsajili beki wa kati wa Sevilla, Mfaransa Jules Kounde baada ya Man United kujitoa katika mbio za kumsajili beki huyo. United sasa wanamlenga zaidi beki wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Raphael Varane, 28. (Dean Jones via Express)

United wanaweza kumtoa kiungo wao Paul Pogba, 28, kama sehemu ya makubaliano ya kumnasa Varane. (AS)

Kocha mpya wa Tottenham Nuno Espirito Santo anataka kukutana na mshambuliaji Harry Kane, 27, ili kujadiliana naye mustakabali wake katika klabu hiyo kabla hajaenda mapumzikoni baada ya michuano ya Euro 2020. Kane amekwishaweka wazi azma yake ya kutaka kuondoka Spurs. (ESPN)

Tottenham pia ipo katika mazungumzo na klabu ya Bologna ili kumsajili beki raia wa Japani, Takehiro Tomiyasu, 22. (Football London)

Manchester United wameachana rasmi na mipango ya kutaka kumsajili winga wa Barcelona Ousmane Dembele, 24. Mfaransa huyo mwenye majeraha ya mguu atakuwa nje ya uwanja kwa miezi minne. (Sport - in Spanish)

Beki wa kati wa Ubelgiji Toby Alderweireld, 32, ameiambia klabu yake ya Tottenham kuwa ana mpango wa kuondoka, na inatarajiwa Spurs haitamzuia kufanya hivyo kama akipata ofa nzuri. (Athletic - subscription required)

Arsenal wanamfuatilia kwa karibu kiungo waSheffield United Sander Berge, 23. Hata hivyo raia huyo wa Norway anawindwa pia na Liverpool, Lazio na Napoli. (Sun)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...