Search This Blog

Monday, July 12, 2021

Takribani watu 20 wauawa Kongo

 


Watu wapatao 20 wameuawa katika mapigano yaliyotokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kati ya muungano wa makundi yenye silaha ya Makanika-Twigwaneho-Ngumino na majeshi ya serikali. 

Msemaji wa jeshi katika jimbo la Kivu Kusini, Kapteni Diedonne Kasereka amesema wanajeshi watano na wapiganaji 15 waliuawa kwenye mapigano hayo ya Jumamosi na Jumapili. 

Kapteni Kasereka amesema wanajeshi waliudhibiti tena mji wa Minembwe jana na amewasihi wakaazi wa eneo hilo waliokimbia mapigano warejee kwa sababu hali imedhibitiwa na jeshi. 

Duru za Umoja wa Mataifa zimeliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kwamba maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Kongo walikesha usiku wa Jumamosi na Jumapili katika kambi ya Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo, MONUSCO



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...