Search This Blog

Friday, July 16, 2021

Rais wa 12 wa Pakistan Mamnoun Hussein, ameaga dunia


Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani ya nchi, Arsalan Mamnoun, mtoto wa Mamnoun Hussein, alitangaza kuwa baba yake alifariki katika hospitali huko Karachi, ambapo alikuwa akitibiwa saratani kwa mwaka.

Mamnoun Hussein ambaye alizaliwa Novemba 23, 1940 huko Agra, India, alianza maisha yake ya kisiasa mnamo mwaka 1969.

Mamnoun Hussein, ambaye ameshika nyadhifa za juu katika taaluma yake ya uongozi ikiwa ni pamoja na ugavana wa mkoa wa Sindh, pia aliwahi kuwa Rais wa 12 wa nchi yake kati ya mwaka 2013-2018.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...