Search This Blog

Friday, July 16, 2021

Gomes achaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Juni


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Juni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania, leo Julai 16 imeeleza kuwa Gomes ameshinda tuzo hiyo baada ya kukiongoza kikosi hicho kushinda kwenye michezo mitatu ambayo walicheza.

Michezo hiyo ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting 0-3 Simba, Polisi Tanzania 0-1 Simba na Simba 4-1 Mbeya City.

Pia amewashinda makocha ambao ni pamoja na Nasreddine Nabi wa Yanga pamoja na George Lwandamina wa Azam FC.

Inakuwa ni tuzo ya pili kwa Gomes kwa kuwa ile ya awali alitwaa mwezi Aprili.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...