Mwanasarakasi wa Kimarekani na mshindi wa medali nne za dhahabu za Olimpiki Simone Biles amejiondoa kwenye fainali za michezo hiyo jijini Tokyo.
Biles, mchezaji wa sarakasi wa Marekani mwenye mafanikio wakati wote, amesema analenga kuzingatia afya yake ya akili baada ya kujiondoa kwenye fainali hizo siku ya Jumanne.
Mkuu wa timu ya Olimpiki ya Marekanina wachezaji wengine wamesifu uamuzi wa Biles kulipa kipaumbele suala la akili yake.
Mchezaji huyo wa miaka 24 alitarajiwa kutetea taji lake Alhamisi,jijini Tokyo.
Timu ya wanasarakasi wa Marekani imesema: "Simone ataendelea kutathminiwa kila siku ili kubaini iwapo atashiriki au la fainali za mchezaji mmoja mmoja wiki ijayo.
"Tunaunga mkono kwa moyo wote uamuzi wa Simone na tunapongeza ushujaa wake katika kutanguliza ustawi wake. Ujasiri wake unaonesha kwanini yeye ni mfano wa kuigwa kwa wengi."

No comments:
Post a Comment