Search This Blog

Friday, July 30, 2021

Mvua kubwa zasababisha uharibifu wa makazi ya watu kwenye kambi za wakimbizi nchini Bangladesh

 


Maelfu ya watu walipelekwa kwenye makazi ya pamoja kufuatia mvua kubwa zilizoharibu nyumba katika kambi za Waislamu wa Rohingya kusini mwa Bangladesh.

Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) la wakimbizi limesema kuwa zaidi ya sentimita 30 za mvua zilinyesha kwenye kambi za eneo la Cox's Bazar, ambazo zina makazi ya Warohingya zaidi ya 800,000.

Ikibainishwa kuwa zaidi ya wakimbizi elfu 5 waliwekwa kwa muda katika makaazi, shirika hilo limesema, "Hali ni ngumu zaidi hasa kutokana na janga la corona (Kovid-19)."

UNHCR ilisema mvua hizo kubwa ziliathiri zaidi ya wakimbizi 12,000 na makazi yanayokadiriwa kuwa 2,500 yaliharibiwa.

Mvua kubwa zaidi zinatarajiwa kunyesha katika mkoa huo ndani ya siku chache zijazo.

Watu sita walifariki katika kambi kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi mapema wiki hii.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...