Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amewaonya raia wan chi hiyo wasiotaka kuchanjwa dhidi ya Corona kusalia majumbani mwao .
Amesema nchi yake imechukua hatua ya kuwachanja wanaotaka kupokea chanjo hiyo huku akiongeza kwamba wasiotaka kuchanjwa wakifa basi yeye hajali .
Amesema raia wanaokataa chanjo ni tisho kwa nchi kwa sababu watakuwa wasambazaji wanaotembea wa virusi hivyo . Katika hotuba kwa nchi yake Duterte amesema;
‘ Kwa wale watu ambao hamtaki kuchanjwa nawaambia msitoke nyumbani kwenu.Ukitoka nyumbani kwako ,nitawaambia polisi wakurejeshe ndani.
Utasindikizwa kurejea kwako kwa sababu wewe ni msambazaji anayetembea wa virusi hivi …Iwapo hutaki kuchanjwa basi usitoke kwako..tuwape chanjo wanaozitaka… na wasiotaka kuchanjwa basi mnaweza kufa wakati wowote,mimi sijali’

No comments:
Post a Comment