Search This Blog

Saturday, July 24, 2021

Mchezaji wa Algeria ajiondoa kwenye Olimpiki baada ya kupangwa na mchezaji wa Israel


Mchezaji wa Judo kutoka Algeria fethi Nourine amepigwa marufuku na atarudishwa kwao kutoka katika michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 baada ya kujiondoa katika mashindano hayo kuzuia kukutana na mpinzani wake kutoka Israel.

Nourine ,30, alitarajiwa kukabiliana na Mohamed Abdalrasool siku ya Jumatatu katika raundi ya kwanza ya pigano la kilo 73.

Akizungumza na runinga ya Algeria , alisema kwamba ufuasi wake wa wanachopigania Wapalestina ndicho kilichomshinikiza kutoendelea na mashindano hayo.

Nourine alijiondoa katika mashindano ya dunia ya 2019 yaliofanyika mjini Tokyo baada ya kupangwa kumenyana na Butbul, ambaye alifuzi raundi ya kwanza.

''Hatukubahatika katika droo iliofanywa tulipangwa na mpinzani kutoka Israel na hivyobasi tukajiondoa katika mashindano.Tuliafnya uamuzi wa busara '', Mkufunzi wa Nourine Amar Ben Yaklif aliambia vyombo vya habari nchini Algeria.

Siku ya Jumamosi , Shirikisho la kimataifa la mchezo wa Judo IJF lilisema kwamba taarifa iliotolewa na wawili hao ni kinyume na filosofia ya bodi hiyo.

Nourine na Mkufunzi wake walipigwa marufuku huku uchunguzi ukifanywa , na kamati ya Olimpiki ya Algeria ikawaondoa wawili hao na sasa 'inapanga kuwarudisha nyumbani'.

Tume ya nidhamu ya IJF itafanya uamuzi wa adhabu ya mwisho watakayotoa , huku wakikabiliwa na vikwazo kutoka kwa kamati ya Olimpiki ya Algeria.

Shirikisho la IJF lilifanya uamuzi huo kulingana na sheria za Olimpiki, ambazo zinasema kwamba hakuna aina yoyote ya mgomo , au siasa , kidini au propaganda za kibaguzi zitaruhusiwa katika eneo la Olimpiki au maeneo mengine.

Mzozo wa Israel na Palestina umekuwepo kwa miongo kadhaa sasa huku hali ya wasiwasi ikitanda tena 2021 huku mapigano kuhusu Jerusalem yakienea hadi mipakani.

Wanariadha kutoka mataifa mengine, ikiwemo Iran na Misri , awali wamekataa kushindana dhidi ya Israeli.

Iran ilipigwa marufuku na shirikisho la IJF kwa miaka minne baada ya kumuagiza Saeid Mollaei kujiondoa katika mashindano hayo ya dunia 2019.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...