Search This Blog

Wednesday, July 7, 2021

Marekani yaonya uchokozi wa Iran unahatarisha mazungumzo ya nyuklia


Marekani na nchi zenye nguvu kubwa duniani zimeionya Iran kuwa hatua yake ya hivi karibuni ya kurutubisha madini ya Urani inaweza kukwamisha mazungumzo ya nyuklia ya Vienna.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Ned Price amesema wanaitaka Iran kutotumia mbinu za kijanja na badala yake iwe tayari kurudi kwa mazungumzo ya Vienna.

Taarifa ya pamoja ya Marekani na nchi zenye nguvu kubwa kiuchumi kuionya Iran imetokea saa chache baada ya shirika la kimataifa la nishati ya Atomiki IAEA, kuripoti kuwa Iran inakusudia kurutubisha madini ya Urani kwa hadi asilimia 20, ishara ya hivi karibuni ya kuonyesha kuwa mazungumzo ya kuunusuru mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 huenda yakakwama. 

Hatua ya Iran ya kurutubisha madini ya Urani inamaanisha kuwa nchi hiyo ya magharibi mwa Asia inakaribia kukamilisha kutengeza silaha za nyuklia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...