Search This Blog

Sunday, July 25, 2021

Maelfu waandamana nchini Italia dhidi ya sheria za corona

 


Maelfu ya watu wameandamana nchini Italia kupinga sera za afya za serikali wakati kukianzishwa sheria kali za kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona. 

Shirika la habari la ANSA limeripoti kuwa watu elfu 3 walikusanyika kwa maandamano dhidi ya cheti cha kidigitali cha Corona cha Umoja wa Ulaya kinachojulikana nchini humo kama pasi ya kijani. 

Gazeti la Corriere della Sera limeripoti kuwa maandamano yalifanyika katika miji ya Milan,Turin na Naples.

Hivi karibuni, serikali ya Italia imeimarisha hatua za kupambana na ongezeko la visa vya maambukizo ya virusi vya corona huku ikiweka masharti makali kwa mikusanyiko kwenye maeneo ya ndani. 

Kuanzia Agosti 6, watu watahitajika kutoa uthibitisho wa chanjo, matokeo yanayothibitisha kutoambukizwa virusi hivyo ama ushahidi wa kupona baada ya maambukizo ili kuweza kushiriki katika dhifa za chakula za ndani ama kuingia katika makavazi na mabwawa ya kuogelea miongoni mwa maeneo mengine ya umma.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...