Search This Blog

Friday, July 2, 2021

Kansela Merkel kulihutubia baraza la mawaziri la Uingereza

 


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anayefanya ziara nchini Ungereza anatarajiwa kulihutubia baraza la mawaziri la nchini humo hii leo kwa mara ya kwanza ambapo kiongozi wa nje amefanya hivyo katika muda wa miaka takriban 25 iliyopita. 

Ziara ya Merkel inazingatiwa kuwa fursa ya kuupiga jeki uhusiano wa kibalozi na Uingereza ambayo ni mshirika mkubwa wa pili wa biashara na Ujerumani. Kwa miaka kadhaa nchi hizo zimekuwa zinazozana baada ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya. 

Kansela wa Ujerumani pia atafanya mazungumzo na mwenyeji wake waziri mkuu Boris Johnson ambapo watajadili janga la maambukizi ya virusi vya corona na njia za kuweka taratibu za usafiri baina ya nchi zao. 

Bibi Merkel anataka taratibu kali ziwekwe katika nchi zote za Umoja wa Ulaya kwa wasafiri kutoka Uingereza, ambako maambukizi ya virusi vya corona aina ya Delta yemeongezeka.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...