Search This Blog

Saturday, July 17, 2021

Hatimaye kamati yaanika makosa sita ya Miss Tanzania


Hatimaye kamati ya Miss Tanzania imeweka wazi makosa sita yaliyosababisha kutenguliwa kwa Miss Tanzania 2020/2021,Rose Manfere kwenda kuwakilisha nchi katika mashindano ya urembo ya dunia.

Miongoni mwa makosa hayo ni pamoja na kuunda menejimenti yake nje ya mkataba, kutofuata maelekezo ya kampuni ya The Look, ambao ni wasimamizi wa mashindano hayo na kufanya matangazo ya biashara.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi Julai, 17,2021na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania,Azama Mwasango alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Mwasango amesema makosa ya mrembo huyo ni pamoja na kutofuata malekezo aliyokuwa akipewa na uongozi wa The Look ambayo ndio kampuni inayosimamia mashindano hayo.

Amesema pia amekuwa hakubaliana na mwongozo anaopewa wa jinsi ya kushirikiana na wadhamini wa shindano kwa mujibu wa mkataba.

“Kwa heshima yake na taji kuna vitu anapaswa afanye na aache, lakini kila anapopatiwa mwongozo sahihi wa kufuata anabisha”amesema na kuongeza.

"Mrembo huyu amekuwa akishiriki matamasha ya watu wengine bila kupata ruhusa ya The Look na wakati mwingine kuomba mialiko jambo ambalo linafedhehesha na kudharaulisha hadhi ya Miss Tanzania kwani kwa hadhi yake inapaswa aalikwe”amesema.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...