Search This Blog

Saturday, July 17, 2021

Anayedaiwa kumchoma mpenzi wake ndani ya nyumba akamatwa


Jeshi la Polisi Kanda Maalum linamshikilia Grace Mushi (25) kwa tuhuma za kumchoma moto ndani ya nyumba aliyekuwa mpenzi wake, Khamis Abdallaah (25).

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Julai 17 na Kamanda wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro imeeleza tukio hilo lilitokea Julai 16 saa nane usiku maeneo ya kwa Mzungu Mbezi Makabe katika Wilaya ya Ubungo.

Amesema mtuhumiwa aliamka usiku na kumfungia ndani Khamis kisha kumwaga petroli na kuichoma moto nyumba hiyo kitendo kilichosababisha kifo cha mwanaume huyo.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha tukio hili ni mgogoro wa kimapenzi,”amesema Muliro.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...