Search This Blog

Tuesday, July 13, 2021

Gabriel Jesus kusajiliwa Juventus


 KLABU ya Juventus imetajwa kuwa imeendelea kukomalia kuipata saini ya mshambuliaji wa Manchester City, Gabriel Jesus.

Habari zimeeleza kuwa Juventus ipo tayari kutoa mkwanja mrefu ili kupata saini ya nyota huyo raia wa Brazil.

Mabosi wa Juventus wanapambana kupata saini ya mshambuliaji matata ambaye ataungana na mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo ndani ya kikosi hicho huku jina la Jesus likitajwa.

Huenda dili la nyota huyo likakamilika kwa sababu amekuwa hana nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza mbele ya Kocha Mkuu, Pep Guardiola hasa kwa msimu wa 2020/21.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...